Luke 9:57-62

57 aWalipokuwa njiani wakienda, mtu mmoja akamwambia Isa, “Nitakufuata kokote uendako.”

58 bIsa akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

59 cIsa akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.”

Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

60 dIsa akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.”

61 eMtu mwingine akamwambia, “Bwana, nitakufuata lakini naomba kwanza nikawaage jamaa yangu.”

62Isa akamwambia, “Mtu yeyote atiaye mkono wake kulima, kisha akatazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
Copyright information for SwhKC